Tafuta

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. 

Kard.Parolin atakuwa Jordan kwa ajili ya kutabaruku Kanisa la Ubatizo wa Yesu!

Papa Francisko amemteua Katibu wa Vatican kuwa Mwakilishi wake katika maadhimisho ya kutabaruku kwa Kanisa la Ubatizo wa Yesu nchini Jordan tarehe 10 Januari 2025.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Katibu wa Vatican  Kardinali Pietro Parolin, kuwa mjumbe Mwakilishi wake kwa ajili ya maadhimisho ya kutabaruku kwa Kanisa la Ubatizo wa Yesu nchini Jordan. Haya yalitangazwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatica iliyotolewa ltarehe 2 Januari 2025. Sherehe hiyo itafanyika tarehe 10 Januari 2025.

Kanisa hilo linalojulikana kama "Bethania ng'ambo ya Jordan" kwa lugha ya wenyeji Al-Maghtas, kihalisi "huzamishwa" -, liko kwenye ukingo wa mashariki mwa Mto Jordan, kilomita tisa kaskazini mwa Bahari ya Chumvi. Maeneo hayo mawili  ni tofauti ya kiakiolojia: Tell Al-Kharrar, inayojulikana pia kama Jabal Mar-Elias kulingana na historia ya  Nabii Eliya aliyepaa mbinguni, na eneo la makanisa ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji  karibu na mto. Hapo inaaminika kwamba ni mahali ambapo Yesu alibatizwa

02 Januari 2025, 17:00