Vituo vipya vya njia ya Msalaba vimezinduliwa katika Basilika ya Mtakatifu Petro
Vatican News
Kama sehemu ya mipango iliyotangazwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka Mia Nne ya Kuwekwa Wakfu kwa Basilika ya Vatican(1626–2026),(Fabbrica di San Pietro), yaani Karakana ya Mtakatifu Petro ilizindua Vituo vipya vya njia ya Msalaba ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro, Ijumaa tarehe 20 Februari 2026, saa Tisa alasiri. Kazi hiyo imefanywa na msanii kijana kutoka Uswiss Manuel Andreas Dürr, aliyechaguliwa kufuatia shindano la kimataifa lililotangazwa mnamo Desemba 2023.
Shindano la Kimataifa
Shindano hilo, lililofunguliwa bila ubaguzi wa utaifa, jinsia, umri, au dini, lilivutia zaidi ya maombi elfu moja kutoka nchi themanini katika mabara matano. Tume hiyo, iliyojumuisha wanahistoria wa sanaa, wanaliturujia, na wawakilishi wa taasisi za Vatican, baada ya uteuzi wa awali kulingana na Wasifu wao(CV) na kwingineko za picha, iliwaalika wasanii kumi na wanne kuwasilisha michoro miwili, ikiwa ni pamoja na ile ya lazima iliyowekwa katika kituo cha kumi na mbili: Yesu anakufa msalabani.
Baada ya tathmini makini, pendekezo la Dürr lilichaguliwa kwa kauli moja kwa usawa wake wa utunzi na nguvu ya kuelezea ambayo inatafsiri Fumbo la Pasaka. Vituo kumi na vinne, vilivyotengenezwa na mafundi wa Karakana ya Mtakatifu Petro, vitakuwepo kando kando ya kuzunguka Ungamo kwa kipindi chote cha Kwaresima, vikihudumia maombi ya waamini na wageni.
Uzinduzi wa Njia ya Msalaba
Saa kumi 10.00 jioni mara tu baada ya uzinduzi mfupi, ibada ya Njia ya Msalaba ilifanyika ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro. Sherehe hiyo iliwaongoza washiriki kando ya vituo kumi na vinne, katika safari ya kutafakari Mateso ya Bwana, pamoja na masomo, sala, na wakati wa ukimya, katikati ya nafasi ya liturujia inayohifadhi kumbukumbu ya Mtume Petro.
Mazungmzo katia ya sanaa na liturujia kwa jumuiya ya Kanisa na mahujaji
Kwa njia hii mpya ya Msalaba, Basilika ya Mtakatifu Petro inasasisha mazungumzo kati ya sanaa na liturujia, ikiwapatia jumuiya ya Kanisa na mahujaji ishara inayoonekana ya jinsi uzuri unavyoendelea kuwa njia ya kupendelewa ya kutafakari fumbo la Msalaba.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here