Tafuta

Maandamano yanaendelea katika jiji la Dar Es Salaam  Tanzania hata baada ya uchaguzi wenye machafuko. Maandamano yanaendelea katika jiji la Dar Es Salaam Tanzania hata baada ya uchaguzi wenye machafuko. 

Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025:Vijana Gen Z, wanaka mabadiliko!

Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025 ilikuwa ni siku ya uchaguzi Mkuu wa Rais na wabunge nchini Tanzania,lakini siku iliyoambatana na maandamano makubwa ya kupinga ambayo hayajawahi kutokea tangu nchi kupata uhuru wake na kuashiria upinzani kwa chama tawala CCM tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi kunako 1992.Siku iliatambatana na kukatika kwa umeme,Intaneti,kuchoma moto vituo mabasi na miundo mbinu,kufyatua risasi za machozi na kukamatwa baadhi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Tanzania uliofanyika Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025, uliambatana na maandamano makubwa kuwahi kutokea tangu Uhuru wake. Ni maandamano yaliyoandaliwa na vijana, kwa kujumuisha miji hasa mikubwa licha ya kukatika kwa umeme, Intaneti na kutolewa hata amri ya kutotoka nje. Hali halisi ya wasi wasi ilianza kujitokeza hapo awali, ambayo ilifikia Kanisa Katoliki nchini Tanzania, kunako tarehe 23 Agosti 2025, kutoa  wito wa Sala na mafungo kwa ajili ya kuombea haki na amani nchini humo. Siku hiyo ilifanyika na baadaye miito mingi imeendalea kutolewa kwa ajili haki na amani. Kabla ya tarehe hiyo kunako mwezi Juni, Baraza la Maaskofu Katoliki,(TEC), katika maadhimisho ya Sherehe ya Pentekoste kwa Mwaka 2025,  walikazia umuhimu wa Watanzania kupenda kutawaliwa na fadhila za kimungu yaani: za haki, amani, ukweli na maridhiano ili kuendelea kulijenga taifa kulingana tunu walizoacha waasisi wa taifa la Tanzania.

Mwalimu Nyerere alituachia Urithi mkubwa wa kujenga amani inayotokana na haki
Mwalimu Nyerere alituachia Urithi mkubwa wa kujenga amani inayotokana na haki

Waliwahamasisha kwamba “Kama raia wa Tanzania, nchi ambayo tunajitapa kama kisiwa cha amani tupende kushughulikia mambo yetu kwa msingi wa ukweli, haki na amani na unaompendeza Mungu ili tuendelee kudai kuwa sisi ni kisiwa cha amani. Katika yale yanayoendelea katika zama hizi katika nchi yetu ninashauri tusithubutu kujiita kuwa ni kisiwa cha amani, tusithubutu kujitanabaisha kama kisiwa cha amani. Tumwombe Mungu atubadilishe, atugeuze, atuongoe na atufanye kweli watu wanaoakisi amani yake. Tumwombe Roho Makatifu atuimarishe.”

Maandamano Tanzania yenye machafuko
Maandamano Tanzania yenye machafuko

Sababu za kufanya maandamamo zilisikika kwa vijana: shida ya kiuchumi, hukosefu wa haki na amani, hutekaji na ukamataji wa watu wasio na hatia. Picha halisi katika mitandao za kijamii, zilionesha uchomaji wa baadhi ya vituo kadhaa katika miji kuanzia Da Es Salaam, na wakati huo Jeshi la Wananchi likijaribu kutuliza ghadhabu, wakati Polisi wakifyatua risasi  na gesi za kutoa machozi ili kutawanya watu, na vijana wengine kuwarushia mawe na mamia ya waandamanaji walikamatwa.

Vijana waandamanaji nchini Tanzania
Vijana waandamanaji nchini Tanzania

Hiki ni kizazi kiitwacho Gen Z ambacho kinakataa hali halisi iliyaoonekana ya nchi.  Kwa njia hiyo hata kwa kukatika kwa umeme na intaneti nchini kote na amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa 12 jioni, Masaa ya Afrika Mashariki na Kati kama ilivyo tangazwa kwenye Televisheni,  maandamano yaliendelea usiku Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, na Morogoro na katika wilaya nyingine. Hatua hii ya kutaka haki itendeke,  si mara ya kwanza duniani kuona vijana wanaingia barabarani kudai haki zao.

Vijana katika maandamani
Vijana katika maandamani

Suala hili lilionekana hivi karibuni pia  huko Nepal kunako mwezi Septemba 2025, ambapo maandamano yaliyoongozwa na vijana  yalimlazimisha Waziri Mkuu K.P. Sharma Oli kujiuzulu baada ya jeshi kukataa kufyatua risasi dhidi ya umati wa watu.


Na hivi karibuni nchini Madagascar, mwezi huu  Oktoba 2025 unaokaribisha kumalizika yalifanyika Maandamano ya vijana yaliyolazimisha Rais Andry Rajoelina kukimbia; Kanali Michael Randrianirina wa kitengo cha wasomi cha CAPSAT alichukua madaraka tarehe 17 Oktoba 2025.

30 Oktoba 2025, 17:35