Tafuta

Kardinali  John Henry Newman atatangazwa kuwa Mwalimu wa Kanisa. Kardinali John Henry Newman atatangazwa kuwa Mwalimu wa Kanisa. 

Walimu wa Kanisa hadi sasa ni 37 miongoni mwao wanawake 4 pamoja na Newman wanakuwa 38!

Tarehe Mosi Novemba 2025,Kardinali Newman atatangazwa rasimi na Papa Leo XIV kuwa Mwalimu wa Kanisa na kufanya idadi ya Walimu wa Kanisa kuwa 38 waliotangazwa ambapo miongoni mwao Wanawake ni 4.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mama Kanisa Katoliki huwatangaza Watakatifu kuwa Walimu wa Kanisa na kuishi na kutangaza mafundisho yao makuu na utakatifu wa maisha, ambao waliakisi na kuelezea imani kupitia maandishi yao na michango yao ya Kitaalimungu na kimaadili. Jukumu lao ni la msingi kwa kuunda na kutetea mafundisho ya Kikristo yote na kuimarisha Majisteri za Kanisa lote Katoliki. Kwa njia hiyo wasi wa kuwa Mwalimu wa Kanisa ni utambuzi wa heshima ambao Kanisa Katoliki linawapatia  watakatifu ambao walionesha uadilifu wa maisha yao, katika kazi zao, uwezo wa ajabu katika kuakisi  na kuelezea imani na mafundisho, kupitia usambazaji wa maarifa au kupitia mchango wao katika tafakari ya za kitaalimungu, kifalsafa.


Kuna vigezo vitatu vya kutoa utambuzi huu: fundisho kuu, linalothibitishwa na maandishi; utakatifu wa uzima, unaotambuliwa na Kanisa kupitia utakatifu; tangazo la Papa au baraza kuu lililoitishwa kihalali. Kwa njia hiyo wadhifa huo  hupewa wale ambao, mara tu mchakato wa utakatifu unapokamilika, wamejitofautisha katika maisha yao kwa mafundisho bora yanayothibitishwa na maandishi yao na ambao, kwa hivyo, wameimarisha mafundisho ya Kanisa kwa kiasi kikubwa, na katika ngazi ya kujinyima na kiroho.

Huu ni utambuzi unaotolewa tu na Papa au Baraza kuu, na hutolewa mara chache sana. Ni katika Muktadha huo ambao Jumamosi tarehe 1 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kumtangaza Mwalimu wa Kanisa, Kardinali John Newman tarehe Mosi Novemba 2025. Hadi sasa walikuwa ni Walimu wa Kanisa 37 miongoni mwake wanawake 

Orodha ya Wakatifu

                                                                                                                             

Hii ni orodha ya Watakatifu waliotangazwa na Mama Kanisa

 

 

 Jina la   Mtakatifu/ke/me

Mwaka wa kifo

 Wadhifa

 Lugha   iliyotumi ka

 Alitangazwa Mwalimu na

Alitangazwa lini

Chanzo

 

  1

Gregori Mkuu

604

Papa

Kilatino

Bonifacio VIII

20.09.1295

CIC(L), VL

Decr., l. III, t. XXII.

 

  2

Agostino wa Ippona

430

Askofu

Kilatino

Bonifacio VIII

20.09.1295

CIC(L), VI,

Decr., l. lII, t. XXII.

 

  3

Ambrose wa Milano

397

Askofu

Kilatino

Bonifacio VIII

20.09.1295

CIC(L), VI,

Decr., l. III,t. XXII.

 

 4

Girolamo

420

Padre

Kilatino

Bonifacio VIII

20.09.1295

CIC(L), VI,

Decr., l. III, t. XXII.

 

 5

Tommaso wa Aquino

1274

Padre

Kilatino

Pio V

11.04.1567

BDP VII

( 1862), pp. 564s.

 

 6

Atanasio

373

Askofu

Kigiriki

Pio V

1568

BrevRom

 

 7

Basilio Mkuu

379

Askofu

Kigiriki

Pio V

1568

BrevRom

 

 8

Gregori Nazianzeno

389

Askofu

Kigiriki

Pio V

1568

BrevRom

 

 9

Yohane  Crisostomu

407

Askofu

Kigiriki

Pio V

1568

BrevRom

 

 10

Bonaventura

1274

Kardinali

Kilatino

Sisto V

14.03.1588

BDP VIII (1863), pp.

1005-1012.

 

 11

Anselmo waAosta

1109

Askofu

Kilatino

Clemente XI

03.02.1720

Clem.XI 00, cc. 1215s.

 

 12

Isidori di Siviglia

636

Askofu

Kilatino

Innocenzo XIII

25.04.1722

TSR II, p. 226.

 

 13

Petro Crisologo

450

Askofu

Kilatino

Benedetto XIII

10.02.1729

TSR II, p. 219.

 

 14

Lone Magno

461

Papa

Kilatino

Benedetto XIV

15.10.1754

Ben.XIV Bull IV,

pp. 98s.

 

 15

Pier Damiani

l072

Kardinali

Kilatino

Leone XII

27.09.1828

DACSR 2 (Rom

1898), pp. 225s.

 

16

Bernard wa Chiaravalle

l 153

Padre

Pio VIII

Latino

20.08.1830

lvIBR.C 18

( 1856), pp. 136· 138.

 

 17

Ilario wa Poitiers

367

Askofu

Kilatino

Pio IX

13.05.1851

ColLac 4

( 1873), pp. 638s.

 

 18

Alfonsi Maria de 'Liguori

1787

Askofu

Kiitaliano

Pio IX

07.07.1871

ASS 6 (1870·

71), pp. 320·

324.

 

 19

Francis wa Sales

1622

Askofu

Kifaransa

Pio IX

16.11.1877

ASS 10 (1877),

pp. 411-415.

 

 20

Cirilly wa Alessandria

430

Askofu

Kigiriki

Leone XIII

28.07.1882

ASS 15 (1882),

pp. 264s. e p. 276.

 

 21

Cirilly wa Yerusalemu

387

Askofu

Kigiriki

Leone XIII

28.07.1882

ASS 15 (1882),

pp. 265-268 e

pp. 277s.

 

 22

Yohane Damasceno

750

Padre

Kigiriki

Leone XIII

19.08.1890

ASS 23 (1890-

91), pp. 255s.

 

 23

Beda Mtumishi wa Mungu

735

Padre

Kilatino

Leone XIII

13.11.1899

ASS 32 (l899- . 1900), pp. 338s.

 

 24

Efrem wa Siro

373

Shemasi

Kilatino

Benedetto xv

05.10.1920

M S 12 (1920),

pp. 457-471.

 

 25

Petro Canisio

1597

Padre

Kijerumani

Pio XI

2 l.05.1925

AAS 17. (1925),

pp. 349-364.

 

 26

Yohane wa Msalaba

1591

Padre

Kihispania

Pio XI

24.08.1926

AAS 18 (1926),

pp. 379-381.

 

 27

Roberto Bellarmino

1621

Kardinali

Kilatino

Pio XI

17.09.1931

AAS 23 (1931),

pp. 433-438.

 

 28

Alberto Mkuu

1280

Askofu

Kilatino

Pio XI

16.12.1931

AAS 24 (1932),

pp. 5-17.

 

 29

Antonio wa Padua

123 l

Padre

Kilatino

Pio XI

16.0 l.1946

AAS 38 (1946),

pp. 200-204.

 

 30

Lorenzo wa Brindisi

1619

Padre

Kilatino

Yohane XXIII

19.03.1959

AAS 51 (1959),

pp. 456-46 l.

 

 3 l

Teresa wa Yesu (Avila)

1582

Mtawaa

Kihispania

Paolo VI

27.09.1970

AAS 63 (1971),

pp. 185-192.

 

 32

Caterina wa Siena

1380

Mtawa wa Tatu

Kiitaliano

Paulo VI

04.10.1970

AAS 63 ( 1971),

pp. 674-682.

 

 33

Teresa wa Mtoto wa Yesu wa Uso Mtakatifu (Lisieux)

l 897

Mtawa

Kifaransa

Yohane Paulo II

20.10.1997

AAS 90 ( 1998),

pp. 930-944.

 

 34

Yohane wa Avila

1569

Padre

Kihispania

Benedikto XVI

07.10.20 l 2

OR 8.-

9. l0.2012, p. 4

[non inA.AS!].

 

 35

Ildegarda wa Bingen

l l 79

Mkuu wa Watawa

Kilatino

Benedikto XVI

07.10.20 l 2

OR 8.-

9. l 0.2012, p. 5

[non in AAS!].

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 36

 

Gregorio wa Narek

1003

Mmonaki

Kiarmenia / Kituruki

Francisko

12.04.2015

 

 

 37

 

Ireneo wa Lione

202

Askofu

Kituruki /

Ufaransa

Francisko

20.01.2022

Doctor Unitatis

 

 

 

31 Oktoba 2025, 09:44